Home FEDHA Unataka kufanikiwa? Acha vitu hivi

Unataka kufanikiwa? Acha vitu hivi

0 comment 110 views

Kuna msemo unaosema “maneno huumba”. Kwa namna moja au nyingine, msemo huu unaweza kusababisha usifanikiwe katika maisha. Kuna umuhimu mkubwa wa kujiwekea mawazo hasi hata pale mambo yakiwa hayaendi sawa. Hakuna ajuaye kesho lakini uvumilivu, ujasiri na kutokata tamaa ni baadhi ya mambo ambayo yamepelekea watu kufanikiwa na kufikia malengo yao.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo  ambayo kila mtu anatakiwa kuachana nayo ikiwa anataka mafanikio.

 Kujihusisha na watu wenye mtizamo hasi

Watu waliofanikiwa huwa hawaoni shida kujihusisha na watu mbalimbali lakini watu hao huwa wanajua muda wa kuacha kujihusisha na watu wenye mtizamo hasi kwa sababu watu hao huathiri mipango na juhudi za kufikia malengo yao. Hivyo usimchukie mtu mwenye mtizamo hasi, unaweza kumsaidia kwa kubadilisha mitazamo yake na ikiwa hakuna mabadiliko yoyote basi kaa nae mbali kwa nia njema.

Kujilaumu

Ni muhimu kutambua kuwa kuelekea katika kutimiza malengo yako lazima utapitia vikwazo mbalimbali ambavyo vitakusababisha ufanye makosa lakini la muhimu ni kujifunza ili hali ukisonga mbele. Kutumia muda mwingi kujilaumu kutasababisha upunguze kasi na juhudi zako hivyo kuchelewesha mafanikio yako. Ikiwa unataka kufanikiwa jifunze kuwekeza jitihada zako katika mambo yenye umuhimu.

Kujifananisha na wengine

Kitu kimoja ambacho watu waliofanikiwa hufanya ni kufananisha hali waliyokuwa nayo hapo nyuma/walipotoka na kufananisha mahali walipofikia ili kujua mapungufu waliyonayo na kuongeza juhudi zaidi ili kuweza kupata mafanikio zaidi. Waliofanikiwa huwa hawana muda wa kujifananisha na watu wengine kwa sababu wanajua kuwa kila mtu ameandikiwa njia yake katika mafanikio, jambo la muhimu ni kujifunza kutoka kwa kila mtu ili kuweza kupata nguvu ya kufanya mambo makubwa zaidi. Hivyo anza kufanya vitu kwa ajili yako na si kwa sababu watu wengine wanafanya.

Kujitenga na watu

Watu waliofanikiwa hupenda kujichanganya na watu wa aina mbalimbali ili kuweza kujifunza, kufurahi na kutengeneza mtandao. Kwa watu waliofanikiwa maisha yao huwa ni zaidi ya kwenda kazini, kanisani, msikitini, na mambo yanayoendana na hayo. Kwao mafanikio ni pamoja na kuwa na muda na familia zao, kupumzika nk. Unaweza kujifunza mambo ya msingi ikiwa utajichanganya na watu.

Usipuuzie malengo yako

Kila siku unatakiwa kuweka kipaumbele malengo yako kabla ya vitu vingine. Mambo mazuri huja kutokana na juhudi hivyo jiwekee utaratibu wa kutenga malengo ya muda mfupi na muda mrefu na ikiwa mipango hiyo haikwenda kama ilivyopangwa basi ongeza jitihada zaidi, omba msaada na endelea kujifunza kila siku.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter