Home FEDHA Wizara ya Maji yaomba bilioni 600/- bungeni

Wizara ya Maji yaomba bilioni 600/- bungeni

0 comment 107 views

Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa amewasilisha mapendekezo ya bajeti ya Sh. 634.19 bilioni katika Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Prof. Mbarawa ametoa mapendekezo hayo bungeni Dodoma na kuhimiza Bunge kuafikiana nayo ili kuwezesha utekelezaji wa miradi pamoja na malengo yaliyopewa kipaumbele.

Katika bajeti hiyo, Waziri Mbarawa amefafanua kuwa Sh. 23.72 bilioni zitatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida wakati Sh. 610.46 bilioni zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo. Kwa upande wa fedha za miradi, Prof. Mbarawa amesema asilimia 57 zitatokana na vyanzo vya ndani na asilimia 43 zitatoka nje.

“Katika fedha za matumizi, Sh. 17.45 bilioni zitatumika kulipa mishahara ya watumishi wa Wizara na Chuo cha Maji na Sh. 6.26 bilioni kwa ajili ya matumizi mengineyo”. Amesema Prof. Mbarawa.

Alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 ya Sh. 697.57 bilioni, Waziri huyo amesema hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu, Wizara ilikuwa imepokea takribani Sh. 16.65 bilioni, ambayo ni sawa na asilimia 68 ya Sh. 24.36 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. 343.48 bilioni sawa na asilimia 51 ya Sh. 673.21 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter