Home FEDHA Zingatia haya msimu huu wa sikukuu

Zingatia haya msimu huu wa sikukuu

0 comment 142 views

Msimu wa sikukuu huwa ni wakati mzuri hasa kwa wafanyabiashara kufanya mauzo zaidi. Mbali na faida ambazo wafanyabiashara hupata, kuna umuhimu kwa watu kujipanga na kutengeneza mpango maalum ili kuhakikisha mtiririko wa kifedha hauathiriki baada ya msimu huu kuisha. Hivyo ili kubaki katika upande salama kifedha hata baada ya sherehe za mwisho wa mwaka inashauriwa kuchukua hatua hizi:

Tenga bajeti maalum kwaajili ya likizo na zawadi, hapa hutegemeana na utamaduni wa mtu. Kuna wengine kipindi cha sikukuu hupendelea kuchukua likizo na kusafiri wengine hupendelea kufanya manunuzi ya zawadi kwa familia na watu wao wa karibu. Hivyo kabla ya kufanya malipo yoyote inashauriwa kuamua ni kiasi gani unapanga kutumia ili kujua kiasi kinachobaki kwaajili ya matumizi baada ya sherehe kwamfano kodi,ada ya shule, usafiri nk.

Tengeneza Orodha maalum, siku zote watu hutumia fedha zaidi ikiwa hawana orodha maalum ya vitu ambavyo wanahitaji (vya muhimu) kununua. Hivyo katika msimu huu wa sikukuu  kabla ya kwenda kufanya manunuzi yoyote jua unataka kununua nini, kwa nani na hata baada ya manunuzi kama fedha zimebaki haimaanishi ununue bidhaa ambazo hazina umuhimu. Kumbuka kuna maisha baada ya sherehe na kwa kuhifadhi fedha zinazobaki unakuwa na uhakika wa kujikimu mbeleni.

Maduka mengi huwa na punguzo maalum la bei katika msimu wa sikukuu. Hio hupelekea bidhaa na huduma nyingi kuuzwa kwa bei ndogo kuliko kawaida. Hivyo zingatia matangazo yanayohusu punguzo la bei katika maduka na kampuni mbalimbali ili kuweza kununua zawadi au bidhaa kwa bei ndogo zaidi. Kwamfano kupitia mitandao ya kijamii biashara nyingi zinatangaza punguzo la bei wengine wanapunguza bei hadi 50%, jambo la msingi ni kuhakikisha unanunua bidhaa zenye manufaa na umuhimu.

Mbali na hayo, ili kuepuka kufanya matumizi makubwa ya fedha katika msimu wa sikukuu unaweza kutumia muda wako na familia baada ya kwenda sehemu ambazo itakubidi utumie fedha. Kwa kushinda na familia hakutokuwa na haja ya aidha kulipia usafiri, kununua chakula, kuweka mafuta kwenye gari nk.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter