Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Tz kuwasilisha Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030

Tz kuwasilisha Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030

0 comment 97 views

Tanzania inatarajia kuwasilisha Taarifa ya Mapitio ya Hiari ya Nchi ya Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, katika Jukwaa la Juu la Siasa la Umoja wa Mataifa.

Taarifa hiyo itawasilishwa Julai 18, 2023, wakati wa mikutano ya Jukwaa hilo inayoendelea, Jijini New York, Marekani.

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Hussein Kattanga ameeleza kuwa hii itakuwa mara ya pili kwa Tanzania kuwasilisha Taarifa kama hiyo ambapo mara ya kwanza ilifanya hivyo mwaka 2019.

Ameeleza kuwa Jukwaa hilo la Juu la Siasa la Umoja wa Mataifa, ni muhimu kwa kuwa Tanzania itapata fursa ya kueleza fursa na changamoto iliyokumbana nazo wakati wa utekelezaji wa malengo 17 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu na kupata uzoefu kutoka nchi nyingine 39 zitakazowasilisha taarifa hiyo.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi 39 kati ya 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa zilizopata fursa hiyo na itatumia nafasi hiyo kubadilishana uzoefu na nchi nyingine zinazoshiriki mkutano huu muhimu,” amesema Balozi Kattanga.

Ameeleza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi na kijamii na kwamba itatumia jukwaa hilo kueleza namna ilivyofanikiwa kupiga hatua za maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo, elimu, afya, maji, amani na usalama wa nchi.

Waziri wa Fedha Dkt.  atawasilisha Taarifa hiyo kwa niaba ya Serikali mbele ya Jukwaa hilo ambapo itajadiliwa na kutoa mapendekezo ya namna ya kufanikisha agenda ya maendeleo ifikapo mwaka 2030 ambapo mambo kadhaa yanatakiwa kufikiwa.

Mambo hayo ni pamoja na kupiga vita umasikini, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, matumizi ya teknolojia, ujenzi wa miji salama, usawa wa kijinsia na mambo mengine.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter