Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI 28,000 wafunzwa ujasiriamali

28,000 wafunzwa ujasiriamali

0 comment 104 views

Kupitia mradi wa majukwaa ya vijana, taasisi ya Arusha Municipal Community (AMCF) na Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) wametoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 28,000 kutoka kata tatu mkoani humo.

Ofisa Tawala Msaidizi wa Shirika la AMCF, Anna Mushi amesema wametoa mafunzo hayo katika kata ya Lemara, Unga Limited na Sokoni One, huku wakilenga kuwasaidia vijana kiuchumi ambapo wamewafundisha njia za uhakika za kuzalisha bidhaa bora zitakazowasaidia kujiajiri. Ameongeza kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwafundisha vijana masuala ya uongozi, utawala bora, mafunzo ya kushiriki katika shughuli za kiserikali kwa ajili ya maendeleo, kutambua fursa zilizopo kwenye jamii na kushiriki katika ngazi za kutoa maamuzi.

“Tunawahamasisha vijana nchini kuwa wajasiriamali wasitegemee kuajiriwa waliopo vyuoni, tuanze kufikiria hili ili serikali inapofanya kampeni ya kuwa na nchi ya viwanda tunawashauri kujiunga katika makundi mbalimbali kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo ambavyo vitaifanya nchi uchumi wake kukua kwa kasi”. Amesema Ofisa huyo.

Kwa upande wake, Ofisa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Arusha, Hanifa Ramadhani ameeleza kuwa halmsahauri hiyo imetoa mikopo ya Sh. milioni 665 kwa vikundi 118 kutoka kata 25 za jiji hilo kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Muongozo wa serikali katika asilimia hizo 10 ya mapato tuliyokusanya. Tunatoa asilimia nne kwa vijana, nne zingine zingine kwa wanawake na asilimia mbili kwa wenye ulemavu”. Amesema.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter