Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Waganda waimwagia sifa Bandari ya Dar es salaam

Waganda waimwagia sifa Bandari ya Dar es salaam

0 comment 120 views

Kufuatia ziara ya Kamati ya Fedha, Mipango na Maendeleo ya Kiuchumi ya Bunge la Uganda katika Bandari ya Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Henry Musasizi amesema kuwa bandari hiyo imefanikiwa kupitisha mizigo yenye thamani ya dola milioni 30 (Bilioni 599 za Uganda) kwa mwaka 2017/2018.

Musasizi amesema hadi sasa. Kamati hiyo imeridhishwa na usafirishaji wa mizigo kutoka nchi nyingine duniani kwenda Uganda kupitia Bandari ya Dar na kuipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) kwa maboresho mbalimbali waliyofanya bandarini hapo.

“TPA inapokea bidhaa; kwa sababu Bandari ya Dar es salaam ni bandari ya kuingia na kuondoka kwa bidhaa zinazoenda nchini kwetu, hivyo TPA imewezesha kufanyika kwa biashara kati ya Uganda na sehemu nyingine za dunia”. Amesema Mwenyekiti huyo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Elihuruma Lema ameeleza kufurahishwa na ugeni huo na kusema mamlaka hiyo imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha mizigo ya Uganda inasafirishwa kwa muda na gharama nafuu.

“TPA pia tumefungua ofisi nchini Uganda ambayo inatusaidia kuwafikia wateja wetu kwa ukaribu, kupokea malalamiko yao, kusaidia katika suala la masoko kwa kupitia Uganda nzima kuangalia wateja tunaowahudumia pamoja na kutafuta wateja wapya ili ili kuongeza mzigo unaopita Bandari ya Dar es salaam kwenda Uganda”. Ameeleza Lema.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter