Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Watanzania watakiwa kumuenzi Lowassa kwa uzalendo na uwajibikaji

Watanzania watakiwa kumuenzi Lowassa kwa uzalendo na uwajibikaji

0 comment 255 views

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema namna bora ya kumuenzi Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa ni kuendelea kuyaishi maono yake ya uzalendo, uwajibikaji ili iwe dira ya kuzidi kujenga umoja na kupiga hatua za maendeleo nchini.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo wakati akitoa salamu za pole na kutoa heshima za mwisho kwa Hayati Lowassa katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam Februari 13, 2024.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ametoa salamu za Pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, familia na wananchi wote kwa msiba huu.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa amejifunza mengi kutoka kwa Hayati Lowassa ukiwemo uzalendo, uwajibikaji, ushirikiano na watu wa makundi yote na kuweka mbele maslahi ya nchi.

Hayati Lowassa alifariki Februari 10, 2024 na anataraji kuzikwa Februari 17, 2024 Wilayani Monduli.

Rais Hussein Mwinyi na Mkewe Mariam Mwingi wakitoa heshima za mwisho kwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter