Home KILIMO Serikali kuchochea uzalishaji pamba

Serikali kuchochea uzalishaji pamba

0 comment 108 views

Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa amesema serikali imepanga mikakati mbalimbali ya kuimarisha zao la pamba ili kuchochea uzalishaji, kuongeza tija na kuimarisha biashara. Naibu Waziri Bashungwa amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara wilayani Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan mkoani Shinyanga.

Naibu Waziri huyo amesema ili kuchochea uzalishaji wa pamba, serikali inatarajia kuanzisha pamba mbegu vipara ili kuachana na matumizi ya pamba manyoya ambayo tija yake ni ndogo.

“Sisi kama Wizara tutakuwa na jukumu la kushawishi wawekezaji ili kuwekeza kwenye viwanda vya pamba nyuzi pamoja na viwanda vya nguo na kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza vyema maelekezo yaliyoainishwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020”. Amesema Naibu Waziri huyo.

Aidha, Naibu huyo amesema watatoa elimu kuhusu matumizi ya pamba mbegu vipara ili kuwajengea uelewa wananchi na kuwezesha serikali kufikia hatua ya kufungamanisha kilimo cha pamba na kufikia azma ya uchumi wa viwanda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter