Bei ya chupa za plastiki imeshuka kutoka Tsh 500 kwa kilo hadi Tsh 250.
Hiyo ni kutokana na wanunuzi wakubwa ambao ni raia wa China kufunga viwanda wakati wa msimu wa sikukuu.
Mnunuzi wa makopo wa eneo la kimara anasema “wachina wamesafiri kwenda China kwa ajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka hivyo wanunuzi wamekuwa wachache na kusababisha bei kushuka”.
Anaeleza kuwa biashara hiyo hushuka mwishoni mwa mwaka ambapo kuanzia mwezi Oktoba bei huanza kupungua hadi kufika mwezi Januari ambapo wanunuzi wa jumla hurudi.
Mmoja wa waokota chupa za plastiki amesema kipindi hiki huwa kigumu kutokana na kushuka kwa bei ya chupa hizo.
“Tulikuwa tunauza hadi chupa za Tsh 20,000 kwa siku lakini kwa sasa ni ngumu kupata iyo ela kwa sababu tunaowauzia wameshusha bei”.
Soma Zaidi: Unaweza kupata Sh 20,000 kwa siku kwa kuuza makopo