Ni dhahiri kuwa miaka 15 iliyopita kampuni ya Motorola ilikuwa ni moja ya kampuni pendwa ya simu hasa kutokana na simu yake ya kujikunja (fold) ya Razr iliyochukua umaarufu miaka ya 2004. Kutokana na hilo Kampuni hiyo imezindua rasmi hapo jana simu janja mpya inayojulikana kama Motorola Razr 2019, yenye muundo kama wa simu za Motorola Razr za zamani huku ikiwa na maboresho ambayo yanaifanya simu hiyo kuingia katika kundi la simu janja zinazojikunja (Foldable smartphones) kwa mwaka huu.
Motorola Razr 2019 imekuwa ni simu ya kwanza kutengeneza katika mfumo wa kujikunja bila kubadilika na kuwa Tablet kama simu nyingine zinazojikunja mfano Samsung Fold. Hivyo hii inaweza kuwa ni fursa kwa kampuni nyingine kubuni simu janja zinazojikunja ili kuweza kuwahamasisha wateja wasiopenda maumbo makubwa sana ya simu zinazojikunja na kuwa katika mfumo tablet.
Hivyo hizi hapa ni sifa za simu hiyo:
- Kioo: simu hiyo inakuja na kioo chenye mtindo wa kujikunja chenye inchi 6.2 chenye teknolojia ya Plastic OLED, kwa nyuma pia kuna kioo chenye inchi 2.7 ambacho kina teknolojia ya G-OLED ambapo kupitia kioo hicho mtumiaji anaweza kupiga simu,picha,kusoma meseji, kusikiliza muziki huku simu hiyo ikiwa imefungwa(imekunjwa). Pia kupitia kioo hicho kinaweza kuonyesha rangi milioni 16 .
- Resolution: 876 x 2142 pixels (~373 ppi density) na 600 x 800 pixels
- Mfumo wa OS: ni Android 9.0 (Pie)
- Prosesa: Qualcomm SDM 710 Snapdragon 710
- RAM: GB 6
- Uhifadhi wa ndani (internal memory): 128GB, hakuna sehemu ya kuweka kadi ya ziada ya kuhifadhia data.
- Kamera: ya Mbele, ina kamera yenye Megapixel 5 ambayo ina uwezo wa kuchukua video za 4K. huku kamera ya nyuma inakuja na Megapixel 16 yenye uwezo wa kuchukua video za 4K.
- Usalama: katika simu hii kuna sense ya kidole ambayo iko mbele (finger print) kwaajili ya usalama wa simu na nyaraka zilizopo ndani ya simu.
- Betri ya simu hii haitoki lakini ina uwezo wa kuchaji kwa haraka
- Rangi: kuna rangi moja tu ya Noir Black
Aidha, simu hiyo itaanza kupatikana Marekani chini ya mtandao wa simu wa Verizon mwezi Disemba mwaka huu, huku ikiuzwa kwa dola za kimarekani 1,500 ambayo ni sawa na Sh milioni 3,462,600 kwa fedha za kitanzania (bei inaweza kubadilika kutokana na viwango vya fedh vya kila siku).
Tupe maoni yako simu hii.