Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) mkoani Tanga Percival Salama ameweka wazi vigezo vitatu ambavyo vitafanya Bandari ya Tanga kuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma bora kati ya bandari zilizopo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati. Meneja huyo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa wiki ya kumbukumbu ya miaka 13 ya huduma za bandari hapa nchini
Amevitaja vigezo hivyo kuwa ni uwepo wa eneo ambalo litafikiwa kwa urahisi na watu kutoka pande zote duniani, uwasilishwaji wa vitendea kazi vya kisasa kutoka Mamlaka ya bandari pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo mkoa wa Tanga.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapa amesema kuwa ili kukomesha vitendo vya upitishwaji wa bidhaa za magendo katika bandari bubu, serikali imeamua kuongeza nguvu na kushirikiana na vyombo vyote vya doria badala ya kutegemea polisi pekee.