Wakati akiwasilisha bajeti ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano, ya mwaka 2019/20, bungeni,Dodoma, Waziri wa Wizara hiyo, Isaack Kamwelwe, amesema kuwa serikali imetega Sh. bilioni 28.79 katika mwaka wa fedha 2019/20 kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya pili hadi ya nne ya mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam.
Kamwelwe, amesema barabara zitakazohusika ni bararabara ya Kilwa kutoka katikati ya jiji hadi Mbagala; Chang’ombe kutoka makutano ya barabara ya Kilwa/Chang’ombe hadi makutano ya barabara ya Nyerere/Chang’ombe, Kawawa kutoka makutano ya barabara ya Nyerere/Kawawa hadi makutano ya barabara ya Mogorogoro/Kawawa na Sokoine Drive ambapo zote kwa pamoja zina urefu wa kilometa 20.3.
Mbali na barabara hizo amesema ujenzi mwingine utafanyika wa flyover mbili pamoja na vituo katika makutano ya barabara ya Mandela/Kilwa na Nyerere/Kawawa.
Pia aeeleza katika awamu ya tatu na ya nne kutakuwa na muendelezo wa upembuzi yakinifu na usanifu wa barabara zilizopoawamu hizo ambazo ni : kwa awamu ya tatu- Uhuru, Nyerere, Bibi Titi, Azikiwe ambazo zina urefu wa kilometa 23.6, na awamu ya nne- Ali Hassan Mwinyi hadi Morocco, na kuendelea Tegeta kupitia Mwenge barabara hizo zina kilometa 25.9. huku zikihusisha barabara ya Sam Nujoma na kuungana na mradi wa mabasi yaendayo haraka awamu ya kwanza kwenye kituo kikuu cha Ubungo.