Home VIWANDAMIUNDOMBINU Mradi wa bomba la mafuta waanza kutekelezwa

Mradi wa bomba la mafuta waanza kutekelezwa

0 comment 114 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Ajira na wenye Ulemavu, Jenifa Mhagama, amesema kuwa serikali imeanza kutekeleza programu ya kuwashirikisha wananchi wa mikoa minane inayopitiwa na mradi wa bomba la mafuta ghafi linalotoka Hoima Uganda hadi Tanga.

Waziri huyo amesema hayo wakati akitoa maelezo ya ziada katika  swali lililoulizwa na Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige.

“Nimthibitishie Mbunge na Bunge kwa ujumla kuwa mradi wa bomba la mafuta ambalo ni muhimu kwa ajira na uchumi wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu inatekeleza programu ya Local Content (Ushirikishwaji wananchi ) katika mikoa yote minane ili wananchi wetu waweze kutumia fursa za mradi wa bomba la mafuta, hili si kwa mradi wa bomba la mafuta pekee, Ofisi ya Waziri Mkuu imeshatoa mwongozo wa ushirikishwaji wa Watanzania katika miradi ya kimikakati na ambayo ni mikubwa ya kipaumbele ili wananchi wetu waweze kutumia fursa za miradi hiyo kujiletea maendeleo” amesema Waziri huyo.

Pia ametaja mikoa ambayo ianufaika na programu hiyo kuwa ni Tanga, Kagera, Shinyanga, Geita, Tabora, Singida, Dodoma na Manyara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter