Home VIWANDAMIUNDOMBINU Wanaoishi mabondeni washauriwa kuhama

Wanaoishi mabondeni washauriwa kuhama

0 comment 125 views

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewasisitiza wananchi wanaoishi mabondeni kuchukua tahadhari na kuanza taratibu za kuhama kwani mvua kubwa zinazoweza kuleta mafuriko zinatarajia kuanza. Makonda amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa, wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kwani hali ya hewa inaweza kuwa mbaya.

“Mkoa wa Dar es salaam umeamua kutoa tahadhari mapema kwa sababu mvua zitakazonyesha safari hii ni kubwa na kama hatua hazitachukuliwa mapema zinaweza kuleta athari hasa kwa waishio maeneo hatarishi kama mabondeni. Napenda kuwasisitiza wananchi wachukue tahadhari, walio mabondeni na wanaoishi kwenye nyumba zilizotitia wahame mapema kabla ya mafuriko”. Amesema RC Makonda.

Makonda amesema kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) tayari imeshatangaza kuwa mvua za mwaka huu zitakuwa kubwa. Aidha, ameonya kuhusu ujenzi holela na utupaji takataka kwenye mifereji na mito akidai ndio chanzo kikubwa cha mafuriko na kuwataka wenye mazoea hayo kuacha mara moja.

Pamoja na hayo, Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuziba viraka kwenye barabara ambazo zimekuwa kero wa wananchi.

“Natoa siku saba TARURA kuziba viraka walivyochimba barabarani kuepusha madhara hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha”. Ameagiza Makonda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter