Home VIWANDAUZALISHAJI Ruksa viwanda vya sukari kuagiza nje

Ruksa viwanda vya sukari kuagiza nje

0 comment 114 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema baada ya kufanya mazungumzo na viwanda vinavyozalisha sukari nchini, serikali inatoa ruhusa kwa viwanda vya sukari nchini kuagiza nje sukari pungufu ambayo ni tani 30,000 pekee na viwanda hivyo kufanya biashara na wafanyabiashara wengine nje ya nchi kutokana na viwanda hivyo kuonyesha juhudi katika uzalishaji. Waziri Hasunga pia ameonyesha kufurahishwa na kazi za viwanda hivyo.

“Kwa kweli tunapongeza kazi ambayo viwanda vyetu vimefanya na vinaendelea kufanya, siku chache zilizopita nilisema wanazalisha tani 320,000 lakini sasa hivi uwezo wao umefikia sasa wanazalisha tani 345,000 kitu ambacho ni kizuri na tunawapongeza sana”. Amesema Waziri huyo.

Mahitaji ya sukari mwaka mzima ni tani 670,000 ambapo viwanda hutumia tani  155,000 na matumizi ya kawaida huwa ni tani 515,000. Kwa mujibu wa Waziri huyo, Bodi ya sukari imetoa ripoti Februari mwaka huu na kubaini kuwa jumla ya sukari iliyopo kwa wafanyabiashara na kwenye hifadhi ni tani 129, 228. Hasunga amevitaja viwanda vitano vinavyozalisha sukari nchini kuwa ni TPC Moshi, Kagera Sugar, Mtibwa, Kilombero na kiwanda kidogo cha Manyara. Viwanda hivyo havizalishi sukari ya viwandani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter