Home VIWANDAUZALISHAJI Serikali yazuia vibali uagizaji sukari

Serikali yazuia vibali uagizaji sukari

0 comment 174 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema kuanzia sasa, serikali haitatoa vibali vya uagizaji sukari nje ya nchi kwa wafanyabiashara pamoja na wazalishaji na kwamba, utaratibu mwingine wa uagizaji utatafutwa. Hasunga amesema hayo wakati akifungua mkutano uliowajumuisha wadau wa sekta binafsi, dhumuni likiwa ni kubadilishana uzoefu na kupata maona kukusu namna bora ya kuongeza mahusiano na vilevile kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP II).

“Wazalishaji wa ndani ndio hao hao wanapewa vibali vya kuagiza. Umewahi kusikia wapi? Wataongeza kweli kasi ya uzalishaji? Na mimi niwaambie kabisa hilo hapa kwangu halipo kabisa kama ni kuagiza nitaagiza mimi”. Amesema Waziri huyo.

Aidha, Hasunga amewataka wazalishaji wa bidhaa hiyo hapa nchini kuja na mkakati na namna ya kuongeza uzalishaji ili nchi iweze kujitosheleza na iache kuagiza kutoka nchi nyingine.

“Kama kuna wafanyabiashara ambao walikuwa wanasubiri baada ya kikao hiki waje kuomba vibali wasahau kabisa, kwangu halipo badala yake nina mkakati wa kuboresha uzalishaji ili tusiagize tena nje”. Amesema Hasunga.

Katika maelezo yake, Waziri huyo ameeleza kuwa mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani 670,000 na viwanda vya ndani vinazalisha tani 320,000. Amewaagiza wazalishaji hao kuboresha uhitaji uliopo badala ya kusaka vibali vya kuagiza bidhaa hiyo nje ya nchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter