Home VIWANDAUZALISHAJI Shirikianeni na serikali mnapopata wageni mashuhuri: Dkt. Abass

Shirikianeni na serikali mnapopata wageni mashuhuri: Dkt. Abass

0 comment 127 views

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amezitaka kampuni za utalii nchini kushirikiana na serikali kutanga utalii wanapopata wageni mashuhuri.

Dkt. Abass amesema hayo wakati wa akizindua msafara wa mwanamuziki na mpiga kinubi maarufu aliyeshinda tuzo za Guiness kwa kufanya onesho katika kilele cha mlima Singla – Himalaya, Siobhan Brady ambae ameongozana na wasanii wengine kutoka nchini Ireland kwenda kilele cha Mlima Kilimanjaro kuweka rekodi ya dunia ya Guiness.

“Nasisitiza kampuni za utalii zinapopata wageni mashuhuri zishirikiane na Serikali katika kutangaza matukio hayo kwa faida ya utalii wa Tanzania.” Amesema Dkt. Abass.

Akiwa na Balozi wa Ireland nchini, Mary O’Neil, wamezipongeza kampuni za Mauly Tours ya hapa nchini na Worldwide Adventure ya Ireland kwa kuratibu tukio.

Aidha, amewasilisha pia salaam na baraka za Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan akisema tukio hilo limepewa heshima kubwa kwa kuona umuhimu wake katika kutangaza utalii kama alivyofanya Rais Samia katika Royal Tour.

“Mna baraka zote na tumewaombea hata kwa mababu mfike salama kileleni ili dunia nzima ijue kwamba juu ya Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania rekodi ya dunia imewekwa kwa mtu kutoka Ireland kufanya tamasha kubwa la kupiga kinubi,” amesema Dkt. Abbasi.

Balozi wa Ireland nchini O’Neill amesema kinubi na nyimbo zitakazoimbwa kileleni ni vitu ambavyo ni sehemu ya utamaduni wa Ireland na kwamba mamilioni ya watu wa nchi hiyo watafuatilia tukio hilo mbashara.
Msanii Siobhan Brady, anasema alipoweka rekodi ya Guiness juu ya kilele cha Mlima Himalaya India kwenye futi 16,000 mwaka 2018, alidhamiria kuja Mlima Kilimanjaro kuvunja rekodi hiyo kwa kukwea futi 19,000.
Jumla ya watu 92 wameanza safari hiyo ya kuelekea kileleni leo Julai 20, 2023 wakiwemo waandaaji wa tamasha hilo pamoja na waongoza wageni.

Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu zaidi barani Afrika ukiwa na urefu wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter