Home VIWANDAUZALISHAJI Ulimwengu unatarajia kuwa na upungufu wa chakula: Rais Samia

Ulimwengu unatarajia kuwa na upungufu wa chakula: Rais Samia

0 comment 83 views

Ulimwengu mzima sasa unatarajia kuwa na tatizo la upungufu wa chakula jambo litakalosababisha mfumuko wa bei.

“Hii ni kwa sababu ya athari za Uviko 19, vita vinavyopiganwa huko Ulaya na kubwa zaidi mabadiliko ya tabia ya nchini,” ameeleza Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza hayo wakati akihutubia katika tamasha la utamaduni lililofanyika Bulabo mkoani Mwanza.

Rais Samia amesema sababu hizi tatu, kwa kipindi cha miaka mitatu minne mfululizo sasa zimefanya nchi zetu kutoweza kuzalisha chakula cha kutosha.

“Na kule kwenye chakula cha kutosha kuna vita, kuna vikwazo vimewekwa kiasi ambacho chakula hakiwezi kutoka kwenda katika maeneo mengine.

Ametaja mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo hayana mipaka kuwa sababu nyingine ya upungufu wa chakula duniani.

Rais Samia amesema matarajio ya ulimwengu kwa sasa mfumuko wa bei ungekuwa asilimia 5 lakini kilichotokea ulimwenguni mfumuko wa bei sasa unaanza kwenye asilimia 10 kwenda mbele.

“Na hii ni kwa mabara yote, iwe Afrika, Asia, Marekani, Ulaya mfumuko wa bei ni mkubwa sana.”

Amesema kutoka na hali hiyo nchi mbalimbali zinachukua hatua mbalimbali kurekebisha ili wananchi wasiumie katika mfumuko wa bei.

“Hadi sasa nchi yetu tumeendelea sana kuzuia mfumuko wa bei kwenye chakula. Unapanda kidogo bei ya chakula tunaweka sawa mahesabu bei zinarudi.

Amesema serikali itaweka jitihada mbalimbali ili kukuza kilimo nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter