Kikundi cha maendeleo ya wanawake kutoka Kenya (MYWO) kimefanya ziara ya kihistoria nchini Tanzania.
Kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Bi. Rahabu Mwikali pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mh. Dan Kazungu walimtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Dar es Salaam na kumpatia zawadi mbalimbali zikiwemo picha na mavazi asili.
Wageni wengine waliokuwepo ni Bi. Getrude Mongella ambaye ni mwanasiasa mkongwe Tanzania na alikua Rais wa kwanza wa Pan African Parliament (2004-2009) na Bi. Muthoni Likimani ambaye ni mwanasiasa mkongwe kutoka Kenya.
MYWO kilianzishwa mwaka 1952 kikiwa na lengo la kuhamasisha maendeleo ya wanawake.