Home WANAWAKE NA MAENDELEO Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania waadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutembelea shule

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania waadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutembelea shule

0 comment 119 views

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walitembelea shule ya Sangu, Mbeya na shule ya Arusha Day, katika kuadhimisha siku ya wananwake duniani na kutoa msaada wa vifaa vya mashuleni.

Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (kulia) akimkabidhi zawadi Mkuu wa shule ya sekondari Arusha Day, Joyce Gyunah katika hafla iliyofanyika jijini Arusha jana. Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani, Wafanyakazi wa Vodacom wametembelea shule hiyo ya wasichana na kuwapatia vifaa kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

Meneja Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini, Magreth Lawrence, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Sangu juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wametembelea shule hiyo na kuwapatia vifaa mbalimbali kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen akizungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Arusha Day na kuwahimiza kusoma kwa bidii, katika hafla iliyofanyika jijini Arusha jana. Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani, kampuni ya Vodacom imetembelea shule hiyo ya wasichana na kuwapatia vifaa kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter