Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani, kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom Tanzania, imewakaribisha wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali nchini Tanzania kujionea utendaji kazi wa kampuni hiyo kwenye upande wa kidigitali.

Mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania PLC, Grace Chambua akizungumza juu ya umuhimu wa elimu kwa wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali za kanda ya kati walipotembelea ofisi za kampuni ya Vodacom jijini Dodoma. Katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, Vodacom iliwakaribisha wanafunzi hao na kuwapatia mafunzo juu ya ufanyaji kazi wa idara na vitengo mbalimbali katika sekta ya mawasiliano.

Meneja Mawasiliano na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Christina Murimi, akigawa vifaa kwa wanafunzi waliotembelea ofisi za Vodacom kujifunza juu ya utendaji kazi wa kidijitali wa kampuni hiyo. Katika kusherehekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Vodacom iliwakaribisha wanafunzi hao wa kike kutoka shule mbalimbali na kuwapatia mafunzo ya ufanyaji kazi wa kidijitali katika idara na vitengo vya kampuni hiyo.