Home VIWANDAMIUNDOMBINU Epuka foleni na Google Maps

Epuka foleni na Google Maps

0 comment 100 views

Hakuna mtu ambaye anapenda kuchelewa kwenda mahali lakini suala la foleni limewapelekea watu wengi hasa wanaoishi katika miji mikubwa kama Dar es salaam kuchelewa na kupelekea athari kwa namna moja au nyingine. Kutokana na maboresho yanayofanyika kila siku katika teknolojia, suala la uchelewaji linaweza kuwa na suluhisho  kutokana na programu ya Google Map.

Programu hii imefanya maboresho makubwa kwa watumiaji na kuwawezesha kujua umbali na muda unaoweza kusafiri, kujua muda mzuri wa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine na hivi sasa kwa kutumia mfumo wa GPS, unaweza kuona foleni iliyopo barabarani pamoja na kasi itakayotumika ili kufika eneo husika.

Jinsi ya kutumia Google Maps

Jambo la kwanza la msingi ni kuwa na programu hii katika simu au kompyuta yako. Mara nyingi katika simu za Android huwa na Gooogle Maps tayari, na ikitokea kuwa haipo katika simu yako ya Android basi hakikisha unaipakua katika Playstore. Kwa wale wanaotumia simu za iOS inatakiwa waipakue kutoka App Store bila malipo yoyote zaidi ya kifurushi cha intaneti.

Baada ya hapo, washa mfumo wa GPS ili kifaa chako kionyeshe mahali ulipo, baada ya kuhakikisha ni mahali sahihi basi katika kipengele kinachofuata, andika mahali uendako. Kwa mfano: Ulipo- Mwenge, Unakokwenda-Posta. Baada ya kuandika hivyo moja kwa moja utaona barabara inayoelekeza jinsi ya kufika eneo unalokwenda kutoka mahali ulipo ikiwa ni pamoja na hali ya foleni.

Ikiwa unatumia kompyuta basi nenda moja kwa moja Google, kisha andika eneo ulilopo kisha chagua katika kipengele cha ramani (maps- huwa ni cha tatu kutoka kushoto juu kabisa). Baada ya kupata google maps  bonyeza sehemu imeandikwa “Directions” ambapo itakubidi uweke eneo unalotaka kwenda. Kama ilivyo kwenye simu baada ya programu hiyo kujua unakotoka na unakokwenda basi itakuonyesha barabara na kiasi cha foleni kilichopo kwa muda huo.

Kwenye kifaa chochote aidha simu na kompyuta, huwa na rangi aina moja zinazoonyesha kiasi cha foleni kilichopo katika barabara. Kwa mfano ikiwa katika barabara husika hali ya foleni ni shwari basi itaonekana rangi ya kijani,  rangi ya njano huashiria hali ya foleni ni ya wastani, huku rangi ya damu ya mzee ikimaanisha kuwa foleni ni kubwa sana.

Ikiwa unataka kujua hali ya foleni kila wakati, basi nenda katika menu ya Google Map kisha bonyeza sehemu imeandikwa Traffic (Trafiki), baada ya kufanya hivyo utaona hali ya trafiki ilivyo katika jiji zima ikiwa ni pamoja na barabara unayotaka kwenda. Pia kuna kipengele cha “Live traffic” na  trafiki ya kawaida. Hivyo unaweza kuchagua unataka kujua trafiki ipi kwa muda huo.

Ikiwa huna ufahamu wa kutosha wa lugha ya kingereza wakati wa matumizi ya programu hii, basi unaweza kubadilisha lugha na kutumia kiswahili kupata taarifa zote.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter