Home BIASHARA Usichojua kuhusu biashara

Usichojua kuhusu biashara

0 comment 125 views

Kuanzisha biashara ni mchakato ambao una changamoto mbalimbali ambazo  ili kupata mafanikio katika maisha huwa kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko na kusonga mbele. Sekta ya biashara ni moja kati ya sekta ambazo zinasaidia kujenga uchumi wa taifa kwa kiasi kikubwa kutokana na idadi kubwa ya watu wanaojihusisha nayo. Biashara ni muhimu kwa wengi na kuna umuhimu wa kuendelea kujifunza kila siku ili kuweza kufahamu zaidi.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo sio kila mtu anajua kuhusu biashara.

  • Biashara ndogo hufafanuliwa kama biashara ambayo ina idadi ya wafanyakazi chini ya 500.
  • Inaelezwa kuwa ni 70% za biashara ndogo huanzishwa na kudumu kwa miaka miwili, huku 50% zikidumu miaka mitano, 33% hudumu kwa miaka 10 na 25%  huendelea baada ya miaka 15.
  • Ili kupata wafuasi/wafuatiliaji katika mitandao ya kijamii, kuna umuhimu wa kuchapisha mambo mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo, unajitangaza kwa watu na kuwafikia wateja wengi zaidi.
  • Sekta zinazokua kwa kasi kwa upande wa biashara ndogo ni pamoja na maduka ya vifaa vya magari, na huduma ya usafi. Ndio maana kila wakati inashauriwa kufungua biashara kutokana na mahitaji ya watu kwani unaweza kuwa na wazo zuri lakini je, lina uhalisia?
  • Biashara ndogo huhamasisha ubunifu mara mbili zaidi ya biashara kubwa. Mara nyingi biashara ndogo huzingatia bidhaa zao kuwa rafiki kwa binadamu na vilevile mazingira.
  • Asilimia 70% ya biashara ndogo humilikiwa na kuendeshwa na mtu mmoja.
  • Inaelezwa kuwa asilimia 50 ya biashara ndogo ndogo hutegemea mikopo ili kujiendeleza.
  • Asilimia 60 hadi 80 ya ajira hutokana na biashara ndogo ndogo. Takwimu hizi hupungua baada ya biashara ndogo kuwa kubwa.

Watanzania wengi leo hii wanaendesha maisha yao kutokana na biashara. Sekta hii imeendeela kuwa mkombozi wa wengi katika harakati za kupambana na janga la umaskini. Jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanywa na serikali pamoja na taasisi binafsi kulinda maslahi ya wafanyabiashara wadogo nazo zimeonekana kuzaa matunda kwa sababu mazingira ya kuendesha biashara hapa nchini yanazidi kuboreshwa ili kuwainua wananchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter