Home LifestyleHealth & Fitness Sanlam Tanzania yawapeleka washindi wa mbio, “Capetown marathon”

Sanlam Tanzania yawapeleka washindi wa mbio, “Capetown marathon”

0 comment 112 views

Kampuni ya Sanlam Tanzania imetoa zawadi kwa washindi wa mashindano yalioisha hivi karibuni yaitwayo “Life is a Marathon competition” na kuwapa fursa ya kwenda kushiriki na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya fainali ya “Sanlam Cape Town Marathon” yatakayo fanyika tarehe 15septemba mwaka huu.

Washindi hao ni Jamia Abdallah na lister Lusulo Pakua. Vile Vile balozi wa Sanalam Maulid Kitenge na wateja wa Sanlam Stephen Mndeme na Innocent Shaku wamepata nafasi ya kushiriki katika mashindano hayo.

Hatua ya kwanza ya mashindano ya “Life is a Marathon competition” yalihusisha washindani kuwasilisha picha na video zao zikionyesha jinsi watakavyo jiandaa kushiriki katika mashindano hayo, baada ya hapo washindi walichaguliwa na kupitia mazoezi mbali mbali ya kujiandaa.

Akizungumza katika hafla ilyofanyika ofisi za Sanlam Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Mr Khamis Suleiman, aliwapongeza wachezaji kwa kujituma kwao na kuwasihi kuonyesha juhudi zaidi katika mashindano yanayokuja.

“Tunafuraha sana kuona jinsi wachezaji hawa walivyofanya vizuri na mkiwa mnajiandakusafirinapenda kuwatia moyo mkafanye vizuri zaidi. Iwe unafanyamazoezi kwa ajili ya mashindano ya mbio au unajifunza kuendesha baiskeIi inabidi uwe na mshirika ambaye atakusaidia kufanikisha malengo yako, na hii ndio ngao yetu hapa Sanlam Tanzania, tumejikita katika kutuoa huduma na bidhaa za kidigitali ambazo zitakusaidia wewe katika hatua zote za maisha.”

Sanlam ilizindua mashindano ya “Life marathon” tarehe 8 Agosti kwa lengo la kuonyesha umuhimu waushirikiano katika kuwezesha watu kufanikisha malengo yao na kuwa na maisha bora, piani moja ya njia ya kampuni ya Sanlam kutambua na kuwapongeza wanamichezo mbali mbali nchini Tanzania

Ikiwa ni mashindano pekee ya marathon yenye daraja la dhahabu barani Africa, Sanlam Cape town marathon huleta pamoja zaidi ya vilabu 23 vya kimataifa na wakimbiaji takribani 15,000 kila mwaka,

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter