Home BIASHARA Faida, hasara za malipo mitandaoni

Faida, hasara za malipo mitandaoni

0 comment 130 views

Katika ulimwengu huu wa kidigitali, imekuwa ni kawaida kwa biashara nyingi kupokea malipo kupitia mitandao ya simu pamoja na mifumo wa malipo kwa kadi za benki. Lengo kubwa la malipo ya mtindo huu ni kumrahisishia mteja kufanya manunuzi hata wakati amabo anakosa fedha taslimu.

Hizi ni faida na hasara za kufanya malipo kwa njia ya mtandao.

Faida

Ongezeko la mauzo: Uwepo wa malipo kupitia mitandao katika biashara humsaidia mteja pindi anapokuwa anataka kufanya manunuzi zaidi. Inaweza kutokea kuwa fedha taslimu alizokuja nazo hazikutosha na anahitaji huduma au bidhaa zaidi hivyo njia mbadala ya kufanya malipo humuwezesha mteja kuendelea na manunuzi ikiwa fedha taslimu zimekwisha. Ni muhimu kwa wafanyabiashara kuweka njia mbalimbali za malipo iLI kufanya mauzo zaidi.

Usalama: Kipengele hiki kipo katika pande zote mbili (kwa mteja na mfanyabiashara) ambapo kwa mteja kuwa na uwezo wa kufanya malipo kupitia mtandao ni dhahiri kuwa anakuwa hana fedha taslimu mkononi hivyo ikiwa matukio ya wizi yatatokea basi fedha zake zitakuwa salama, na kwa mfanyabiashara kupokea malipo kwa mtandao anajiepusha na matukio ya wizi au kupoteza fedha.

Mtiririko wa fedha huongezeka: Malipo kwa njia ya mtandao hufanyika kwa haraka na moja kwa moja. Kutokana na hilo, hakuna masuala ya kukopesha au kusubiria taasisi ya fedha kuruhusu muamala ufanyike. Kwa kufanya malipo kupitia mtandao mtiririko wa fedha katika biashara utakuwa unaenda kwa kasi na mwenendo wa biashara unakuwa katika hali nzuri.

Hasara

Gharama za ziada: Wakati wa kufanya malipo katika mitandao mtumaji (mteja) hukatwa kiasi fulani cha fedha kama ada hivyo hii inaweza kuwa changamoto kwake. Pia kwa upande wa mfanyabiashara ikiwa anataka kutoa fedha hizo, lazima akatwe kiasi kadhaa cha fedha hali ambayo inafanya wafanyabiashara wengi wafurahie zaidi malipo ya fedha taslimu kuliko malipo katika mitandao.

Hitilafu katika mtandao: Sio kila wakati mtandao unaweza kuwa sawa, na kuna muda mitandao ya simu hutuma ujumbe kwa wateja wao kuwaelezea kuwa marekebisho yanafanyika hivyo hakutokuwa na huduma. Hii inaweza kumsababisha mteja kushindwa kununua bidhaa ikiwa hitilafu imetokea na mfanyabiashara anaweza kukosa fedha kutokana na hilo.

Kama mfanyabiashara ni muhimu kuwa na njia mbadala ili kurahisisha upatikanaji huduma kwa wateja. Aidha, ni muhimu kusikiliza wateja, na kufanyia kazi maoni yao ili kupata mafanikio zaidi. Kwa  kiasi kikubwa, teknolojia imeendelea kurahisisha shughuli mbalimbalikwa upande wa biashara hivyo hakikisha hubaki nyuma ili kuepuka kupoteza wateja.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter