Home AJIRA Badilisha wazo la biashara kua biashara halisi

Badilisha wazo la biashara kua biashara halisi

0 comment 139 views

Ni kipindi sasa toka umekua na ndoto ya kufanya biashara, ama ya kufanya jambo litakaloweza kukuinua kiuchumi ama kubadili kabisa jambo ulilokua ukilifanya kwa udogo kwenda kwenye hatua nyingine kubwa na hata kuweza kubadili mwenendo wa biashara yako kabisa.

Katika jambo hili la kuanzisha ama kuendeleza biashara yako jaribu kuzingatia yafuatayo.

 

  • Weka malengo.

Ili wazo la biashara litoke kwenye ndoto kuja kwenye uhalisia ni lazima uwe na malengo ya jambo lolote lile unalotaka kuanza ni lazima ujue ni kwa nini unalitaka jambo hilo,na unataka kufikia lengo lako baada ya muda gani,au kwa muda gani.

Wafanyabiashara walioendelea au wanaofanya biashara kwa malengo mara zote hutumia maandishi kama kumbukumbu,haswa kutaka kujua anataka kufanya nini,ni wapi anataka kufanyia biashara yake na itamghalimu kiasi gani,ili tu asipoteze kumbukumbu ya anachokifatilia,Maana Mali bila Daftari,hupotea bila Habari!

 

  • Fanya utafiti.

Kabla ya kua umeanza biashara yako,ni vyema ukafanya utafiti kuhusia na bidhaa unayotaka uiingize sokoni,ama biashara unayotaka kufanya je changamoto zake ni zipi,ni nini unahitaji ufanye baada ya kua tayari umefanya utafiti wa kutosha ili tu usiingie biashara usiyokua na mawazo au ushauri kutoka kwa watu wanaofanya biashara ya aina unayotaka kufanya.Hivyo utafiti utakufany awewe ujue unaanzia wapi.

 

  • Weka akiba.

Njia nyepesi ya kufikia malengo yako ni kujiwekea akiba ya pesa.Hii itakufanya uwe na nidhamu ya fedha na njia pekee ya kujua kiasi gani unaweza ukatunza ili kufikisha malengo yako.Hii haijalishi unapata kipato kikubwa ama kidogo ni lazima uchukue hatua na kutunza asilimia kiasi ya kipato unachopata ama unachoweka.

 

Lipa madeni.

Hii inaweza ikawa tatizo katika biashara endapo tu utaruhusu kuanza biashara ukiwa na madeni,umepata wazo tayari,hakikisha biashara yako aiendeshwi ili kulipa madeni,maana itakua ngumu sana kukua kama tu utatumia pesa ya mtaji au biashara yako kulipa madeni.Ni bora ukawa uko Debt free kabla hujaanza biashara yenyewe.

 

  • Wekeza pesa.

Baada ya kua umeyafanya hayo yote,kinachofata ili biashara yako ikue zaidi ni kuwekeza pesa kwenye biashara yako au vitega uchumi vyako vingine.Pia unaweza ukaweka pesa kwenye mali zinazoweza kuwa zianapanda thamani kila kukicha,kama nyumba ama viwanja!

Kwa kufanya haya na uvumilivu katika kila jambo ulifanyalo linakufanya uweze kufanikiwa katika biashara yako.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter