Home FEDHAHISA Lijue soko la Hisa. Sehemu ya Pili

Lijue soko la Hisa. Sehemu ya Pili

0 comment 45 views

Kutoka kwenye muendelezo wa mada ya Lijue soko la Hisa.

Mada iliyopita tulipata kufahamu nini maana ya hisa, pia tuliangazia tofauti kati ya primary market na Secondary Market. Kama hukupata nafasi ya kusoma unaweza rejea mada iliyopita ili kufahamu zaidi.

Sasa basi leo tutaelezea mambo ya kuzingatia kabla ya kunua hisa na faida anazopata mtu anayemiliki hisa.

Kabla ya kununua hisa ni vyema ukaangalia mambo yafuatayo.

Hali ya Utendaji wa kampuni.

Hapa swali la kujiuliza ni Je, Kampuni inafanya kazi vizuri kwa weledi na inamategemeo ya ukuaji kwa muda mrefu. Kama kampuni itaonesha kuwa na utendaji mzuri unaridhisha na kuonesha hali ya ukuaji basi hiyo kampuni ni sahihi kuwekeza.

Bei ya hisa na uimara wake
Ni muhimu kutazama bei ya hisa na mwenendo wake mfano unaweza kuangalia miezi kadhaa au miaka kadhaa nyuma hisa zilikuwa zikipanda au kushuka kwa uwiano gani.

Wakati wa kununua hisa
Ni muhimu pia kuangalia ni wakati gani unanunua hisa, mfano wakati ambao hisa ndio zinaingizwa au kuuzwa kwa mara ya kwanza kwenye soko la hisa bei huwa ni ndogo sana na baada ya hapo mara nyingi bei huongezeka ingawa kuna wakati hushuka pia.

Wingi wa makampuni katika soko la hisa.

Mfano kuna mabenki zaidi ya matano hii inamaana benki hizi zinagombea wateja hii ni kwa wateja wote wale wanaowahudumia na wale wa kwenye soko la hisa hivyo bidhaa zao zipo za kutosha na bei itakuwa ya kawaida mambo ya demand na supply.

Zifuatazo ni Faida za kumiliki hisa

Gawio

Ukiwa mmiliki wa hisa utapata gawio ikiwa kampuni itapata faida katika kipindi hicho cha mwaka na wanahisa wakaridhia utoaji wa gawio. Gawio hutolewa mara mbili au moja kwa mwaka kutokana sera ya kampuni na maamuzi ya wanahisa.

Ongezeko la thamani

Wanahisa pia huweza kupata faida itokanayo na ongezeko la thamani iwapo bei ya hisa itaongezeka kwenye soko la hisa. Ikiwa ulinunua hisa moja kwa Tsh 800 na baada ya mwaka hisa hizo sokoni zikauzwa kwa Tsh 1,400 basi unakuwa umepata ongezeko la thamani ya shilingi 600 kwa kila hisa. Hii ni faida tofauti na gawio, ikiwa utawekeza katika kampuni nzuri utapata gawio na ongezeko la thamani ndani ya mwaka mmoja.

Vile vile ikiwa bei itashuka na kufikia Tsh 600 utapata hasara ya Tsh 200. Ila ukiwekeza katika kampuni nzuri ni vigumu kupata hasara na unakuwa na uhakika wa bei kuongezeka kwa 20% au 40% au zaidi kwa mwaka.

Huokoa muda wa usimamizi
Ni uwekezaji ambao humpatia mwekezaji uhuru wa kufanya shughuli nyingine na kwa wale ambao hawana muda wa usimamizi katika biashara huu ni uwekezaji mzuri kwao.

Ni mali inayohamishika kwa urahisi
Ni mali ambayo inahamishika ki urahisi na kwa haraka pale mwekezaji anapohitaji pesa yake kwa ajili ya shughuli nyingine. Pia hisa unaweza kuitumia kama dhamana.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter