Home VIWANDAMIUNDOMBINU Agizo la Rais kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja

Agizo la Rais kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja

0 comment 131 views
Na Mwandishi wetu

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ufungaji wa mita za kupimia mafuta kati ya Bandari za Dar es salaam na Tanga kama ambavyo aliagiza Rais Magufuli utachukua muda wa mwaka mmoja baada ya wakandarasi wa kufanya hizo kupatikana. Prof. Mbarawa amedai kazi hiyo siyo rahisi kama watu wengi wanavyodhani hivyo itachukua muda mrefu kutokana na uwepo wa taratibu nyingi.

Waziri huyo ameyasema hayo jana baada ya kufungua Kongamano la Global Logistics la mwaka 2017 jijini Dar es salaam ambalo lilikutanisha mawakala 250 wa forodha kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kujadili namna ya kuboresha miundombinu ya bandari, kukuza biashara na kujenga mahusiano mazuri.

Ameongezea kuwa katika kutekeleza agizo hilo la Rais, wakandarasi 63 wamejitokeza ambapo 35 kati yao wameomba zabuni ya kufunga mita katika Bandari ya Dar es salaam huku 28 kati yao watafanya hivyo katika Bandari ya Tanga. Prof. Mbarawa ameongeza kuwa endapo mkandarasi atawahi, atatumia muda usiopungua miezi tisa kukamilisha mradi huu.

Kuhusu kongamano hilo Waziri Mbalawa amedai mawakala hao wa forodha wamekutana ili kujadili namna ya kuimarisha mahusiano, kupunguza usumbufu katika bandari husika na pia njia mbalimbali za kuboresha huduma zao kwa wateja.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter