Home Elimu UNAJUA FAIDA ZA KUFAHAMU LUGHA ZAIDI YA MOJA KATIKA MAISHA YAKO

UNAJUA FAIDA ZA KUFAHAMU LUGHA ZAIDI YA MOJA KATIKA MAISHA YAKO

0 comment 180 views

Kujifunza lugha mpya sio kitu rahisi,lakini kuna faida nyingi sana kwa mtu anayefanikiwa kujifunza lugha zaidi ya moja.

Kila mtu anajifunza lugha fulani kwasababu zake tofauti na mwengine.Kama unaenda mahali fulani halafu ukashindwa kuwasiliana na wenyeji,hata kuishi kwako kutakuwa kugumu sana.

Unapochukua uamuzi wa kujifunza lugha tofauti au  nyingi kuna watu wasioelewa wataona kama unajishaua hivi,lakini usijali kuonekana hivyo kwani faida zake utakuja kuziona wewe na sio wao.Sidhani kama utafurahia,endapo utakutana na mtu ambaye hamuelewani lugha hata kidogo,na wewe unahitaji msaada kutoka kwake.Katika mazingira haya utakuwa kama nguo ambayo inatembea bila mwili.

Lakini hapa tutaangalia faida tano za kujifunza lugha mpya.

1.KUZIFAHAMU TAMADUNI NYINGINE

Watu wanaofanikiwa kutambua tamaduni zaidi ya moja wanakuwa waelewa wa mambo mengi sana vichwani.

Kwani wanauwezo wa kwenda taifa lolote ambalo lugha yake wanaijua na kufahamu namna ya kuwasiliana na wenyeji katika kutambua utamaduni wao ukoje na kupata huduma muhimu kwa urahisi.

2.KUJUANA NA WATU WA MATAIFA MBALI MBALI

Watu wengi hupenda kukaa karibu,na mtu mwenye uelewa wa mambo mengi kwani wanajua kuna kitu cha kujifunza kutoka kwa mtu huyo.

Wengi wanapenda kusikia taarifa mpya ambazo wao kabla hawakuweza kuwa nazo kutoka katika mataifa mengine.

Na wanaposafiri nchi nyingine inakuwa rahisi kwao kuelewana na wenyeji na pia kupendwa kwani ataonekana ana taarifa mpya ambazo watu wengine wangependa kujifunza.

3.RAHISI KUWA MGUNDUZI WA VITU VIPYA

Utafanikiwa kugundua vitu vingi vipya katika nchi uliyotembelea na kuvileta katika nchi yako na kuwa mgunduzi wa kwanza nchini kwako.

Kwani taarifa nyingi muhimu ambazo unapaswa uzifahamu zinakuwa katika lugha ya kigeni.

4.KUKUZA UWEZO WA KUELEWA NA KUMBUKUMBU

Unapojifunza vitu vipya unafungua nafasi kwa ubongo wako kuongeza uwezo wa kutafsiri mambo mapya na kuyashika kichwani.

Kwani zoezi la kujifunza lugha mpya linakutaka uwe na uwezo mkubwa wa kuhifadhi maneno hayo bila kusahau mapema na hivyo kukujengea uwezo mkubwa wa kumbukumbu.

5.INAONGEZA FURAHA

Sababu mojawapo ya kujifunza lugha mpya ni kukuongezea furaha katika maisha.Unapojua lugha nyingi unaongeza wigo wa wewe kuzifahamu taarifa nyingi zitakazo kuongezea furaha katika maisha yako.

Unapojifunza lugha mpya kama haufurahii kuijua itakuwa ndoto kuifahamu kabisa.

 

*Sasa ushafahamu japo kwa ufupi faida za kujifunza lugha mpya,itakuwa ni vyema kama utajitokeza na kwenda kujifunza lugha mpya.

Kujua lugha yako tu haitakufanya wewe uonekane ndio mzawa kuliko wengine,

lakini kama unaangalia mbali,utagundua mipaka ya mataifa imefunguka kila mahali.Watu wa mataifa tofauti wanazidi kufahamiana.Hali hii huongeza fursa za kufanikiwa katika maisha.

KUJUA LUGHA MOJA TU,SI KITU CHA KUJIVUNIA KATIKA MAISHA YETU.KWANI LEO TUPO HAPA NCHINI NA KESHO HUTUJUI TUTAANGUKIA ENEO GANI LA DUNIA HII AMBAYO MPAKA SASA IMEKUWA KAMA KIJIJI KIMOJA.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter