Home BIASHARA TAMBUA NJIA SAHIHI ZA KUKUFIKISHA KATIKA MALENGO YAKO

TAMBUA NJIA SAHIHI ZA KUKUFIKISHA KATIKA MALENGO YAKO

0 comment 130 views
“Je, niko katika njia sahihi?”Kama, umewahi kujiuliza hili swali,uko karibu kuipata njia yako sahihi.Wengi tunajihusisha katika shughuli mbali mbali bila kujua kama njia tunayoifuata/tuliyochukua ni sahihi au si sahihi kwetu.
Ulishawahi kuamka usiku mnene,huku ukijiuliza kama njia uliyaochagua ni sahihi kwako au la?
Wengi tunajiuliza,kuwa njia sahihi maana yake ni nini?Kujiuliza swali hili,ni hatua kubwa sana kupiga katika maisha yako ya kutafuta shughuli sahihi ya kufanya.Fahamu wazi, kuwa unaanza kujitambua,na ni ishara mojawapo ya kujua mahitaji gani ni muhimu kwako.
Yawezekana,ukawa unalipwa vizuri,mazingira mazuri ya kazi,au una vifaa vyote vya kufanyia kazi zako.Linapokuja suala la upo sehemu sahihi au sio sahihi masuala hayo niliyotaja hapo juu huwekwa kando.
Ishara za kuangalia kama upo njia sahihi katika shughuli unayofanya:
1.MUDA HAUKUTOSHI
Unapokuwa unafanya hiyo shughuli,unaona muda kama unapaa.kuwa kwako si kazi tu bali unafurahia kila dakika ya kitu unachofanya.Na unapokuwa mbali na shughuli yako au 
hata ukiwa umelala unatamani asubuhi ifike ili urudi tena eneo lako la kazi.
2.UNAPOTEZA MUUNGANIKO NA MATUKIO YA NJE YA KAZI
Unapokuwa mzigoni unahisi kama unasafiri dunia ya kipekee,na unapoteza mawasiliano na dunia inayokuzunguka.Unaweza  ukawa unaongeleshwa na watu na usiwasikie kabisa, kwa kuwa akili yako yote imetekwa kwa muda huo na muda mwengine hata kula unasahau.
3.UNA IMANI NAYO MOYONI
Moyoni una imani kuwa hii ndiyo kazi uliyoumbwa kuifanya na hakuna atakayeweza kukubadilisha mawazo na imani yako uliyonayo juu ya shughuli hiyo.
4.UNA MAONO NA SHUGHULI HIYO
Una maono ya wazi kabisa ,ya nini kutaka kupata baada ya muda fulani, na hata kama kuna
vikwazo vinajitokeza bado unanguvu za kutaka kufikia lengo lako.
5.HAUKATI TAMAA
Hata kama kuna watu, au mazingira yanataka kukurudisha nyuma bado hutaki kukata tamaa na 
shughuli yako.
6.UNAFURAHIA CHANGAMOTO
Pamoja na changamoto zinazojitokeza mara kwa mara unafurahia uwepo wake kwani zinakupa
uzoefu mpya ambao mwanzo
 hukuwa nao.
7.WATU WANAKUUNGA MKONO
Watu kadhaa watachukua muda wao,kuwasiliana na wewe ili kukupa msaada na muongozo wa
shughuli yako.
Hata wewe mwenyewe huelewi watu hawa wanakujaje katika maisha yako lakini wanakuja na msaada mkubwa sana kwako.
8.UNACHOFANYA KINALETA MABADILIKO YA KWELI KATIKA MAISHA YA WENGINE
Wewe unaweza ukaona unachofanya ni kitu kidogo lakini kuna watu kinawasaidia sana,
na mrejesho wao utakupa picha halisi ya jinsi unavyogusa maisha ya watu wengine.
NI VYEMA UKAANZA KUJITAFAKARI SASA,KAMA NJIA UNAYOTAMANI AU ULIYOCHUKUA 
NI SAHIHI AU LA.
HII ITAKUSAIDIA KUKUEPUSHA NA UPEPO USIO SAHIHI.NA KUANZIA LEO,TAMBUA KUWA NJIA SAHIHI.
NDIO ITAKAYOKUPA MAFANIKIO YA KWELI KATIKA MAISHA YAKO.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter