Home FEDHA Moto wa sido waleta hasara ya Bil. 14

Moto wa sido waleta hasara ya Bil. 14

0 comment 125 views

 

Na Mwandishi wetu

Baada ya Tume iliyoundwa kuchunguza ajali ya moto ilioteketeza soko la Sido jijini Mbeya siku chache zilizopita kukamilisha uchunguzi wao, Mwenyekiti wa tume hiyo Hassan Mkwawa amesema chanzo cha moto huo ni shughuli za matumizi ya moto ndani ya soko hilo na kwa mujibu wa uchunguzi huo, ajali hiyo imesababisha hasara ya takribani bilioni 14.2.

Mkwawa ameongeza kuwa uchunguzi wao uligundua mabaki ya moto yaliyokuwa tofauti na yale ya moto wa mabanda hivyo kudhihirisha kuwa kulikuwepo na moto uliokuwa ukihifadhiwa baada ya mamalishe kumaliza shughuli zao. Ameshauri serikali kuchukua tahadhari na kuweka utaratibu maalum ili kuepusha ajali kama hii katika masoko mengine.

Akizungumza kwa niaba ya serikali, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amesema wafanyabiashara walioathirika na ajali hii hawatahamishwa bali watabakia mahali hapo kwa masharti ya kujenga vibanda vya kudumu na kufuata mchoro watakaopewa na wataalamu.

Naye Naibu Spika wa Bunge hapa nchini  Dk. Tulia Ackson pamoja na kutoa msaada wa milioni 10 kwa waathirika wa soko, amewaomba wananchi hao waendelee kuwa watulivu na kuongeza kuwa viongozi wa serikali wanatambua umuhimu wa shughuli zao katika maendeleo ya taifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter