Home BIASHARAUWEKEZAJI Diaspora washauriwa kuwekeza nchini

Diaspora washauriwa kuwekeza nchini

0 comment 58 views
Na Mwandishi wetu

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema serikali za Jamhuri wa muungano wa Tanzania pamoja na Zanzibar zimelenga kuwapa nafasi kubwa watanzania walio nje ya nchi (Diaspora) ili wapate fursa ya kuchangia maendeleo ya nchi, hasa katika masuala ya uwekezaji. Samia amesema katika hotuba ambayo ilisomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira) January Makamba  kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Diaspora unaofanyika Kaskazini B, Unguja.

Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuweka mazingira rafiki kwa kwa jamii ya watanzania hawa wanaoishi nje ya nchi ili wao pia washiriki na kuchangia pato la taifa. Amewataka watanzania hao kuwa raia wema wanapokuwa nje ya nchi. Pia ameshauri washirikiane na serikali ili kujadili changamoto zinazowakabili ambazo zinarudisha nyuma jitihada zao za uwekezaji.

Hivi karibuni, Serikali ya Jamhuri ya Muungano imezindua ofisi sita za ubalozi wa Tanzania nje ya nchi kama njia mojawapo ya kutoa fursa kwa watanzania kuwasiliana na nchi yao bila usumbufu wowote.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter