Home FEDHA UMUHIMU WA MSHAURI WA FEDHA KATIKA BIASHARA

UMUHIMU WA MSHAURI WA FEDHA KATIKA BIASHARA

0 comment 127 views

Teknolojia zinaendelea kuboreshwa na kurahisisha masuala mengi duniani. Siku hizi imekuwa rahisi kupata taarifa mbalimbali na kujifunza kwa njia ya kiektroniki kama simu. Elimu ya fedha ni muhimu hasa kwa watumiaji na kadri watu wanavyojifunza kuhusu fedha idadi ya maskini pia inapungua kwa sababu watu wengi wanaendelea kuwa na uelewa kuhusu usimamizi wa fedha na mambo ya kufanya na kutofanya ili kujenga uchumi imara.

Japokuwa aarifa zimerahisishwa, kuna umuhimu wa kukutana na mshauri wa fedha ikiwa unaona mambo hayaendi, kwani sio kila kitu kinapatikana katika mtandao na kutokana na mwenendo wako kifedha, mtaalamu anaweza kusaidia kwa upana zaidi.

Mshauri wa fedha ana mchango mkubwa kama inavyoelezwa hapo chini:

Uthibiti wa habari. Habari hutuwezesha kufanya maamuzi sahihi. Lakini zinaweza kutuchosha pia kwasababu si kila mtu anapenda kusoma na kufuatilia mambo. Upatikanaji wa habari kwa urahisi ni jambo zuri, pia kuwa na habari haimaanishi ndio kuelewa. Ikiwa habari zinatuogopesha kufikia maamuzi katika kutenda jambo basi ni muhimu kupata mshauri, hapo ndipo wataalamu wanatakiwa kuhusishwa. Katika fedha kazi ya mshauri ni kuhakikisha kuwa anarahisisha taarifa kwa kuelezea kwa urahisi ili mhusika aweze kuelewa na kujua nini cha kufanya kulingana na malengo na uwezo wa kifedha.

Uchaguzi mwingi

Sio kila mtu ana muda wa kuchagua wapi kwa kuwekeza fedha zake, ndio maana wataalamu ni muhimu. Ikiwa huna muda wa kufanya utafiti kuhusu uwekezaji ni muhimu kumuajiri mshauri wa fedha kwa sababu huwa wana orodha ambayo tayari wameshaifanyia utafiti. Ikiwa unapata shida ya kufanya uchaguzi ni vyema ukamtafuta mtaalamu wa masuala ya fedha ili kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Muda mchache

Kama una majukumu mengi sio vibaya ukielekeza baadhi ya mambo kwa wataalamu ili kuepuka kupoteza muda hasa kwenye mambo usiyokuwa na uelewa nayo. Kwa kujihusisha zaidi kwenye mambo unayoyaelewa zaidi kutasaidia na watu wengine watekeleze pande zao. Hivyo kama unafundishwa au mwanasheria elekeza nguvu na muda kwenye mambo hayo huku ukiajiri watu wengine kwa muda mfupi au moja kwa moja ili waweze kusaidia.

Ukosefu wa utaalamu

Kama ilivyo katika tasnia mbalimbali, kila mtu huwa na utaalamu wake. Hata wataalamu wa fedha hubobea katika mambo mbalimbali kwa mfano kuna wataalamu wa fedha waliobobea katika biashara, muda wa mapito, mipango ya talaka huku wengine wakijikita katika sekta maalumu. Ili kufanya maamuzi sahihi ni vyema kuwasiliana na mtaalamu aliyebobea katika kipengele husika.

Kujipendelea

Kusimamia fedha zako mwenyewe kuna hasara na faida. Ni kweli kutakusaidia usitumie gharama nyingi ya kuajiri mtu. Lakini ni muhimu kujua kila mtu huwa na hali ya kujipendelea na kutumia hisia kufanya maamuzi. Kuwa na mshauri hurahisisha kufanya maamuzi kutokana na hisia, mshauri atakushauri kutokana na hali halisi.

Kama unaona unaweza kufanya maamuzi kuhusu fedha zako, una uelewa na ujuzi na mambo ya fedha na una uwezo wa kufanya maamuzi bila kujali sana hisia zako basi si jambo baya. Lakini kama una mambo mengi na huna muda wa kujihusisha na mtiririko wako wa fedha basi si vibaya ukamuajiri mshauri ili mambo yaende.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter