Virusi vya Corona ni moja kati ya familia kubwa ya virusi ambayo ni vya kawaida kwa wanyama. Wakati mwingine, watu huambukizwa na virusi hivi ambazo vinaweza kuenea kwa watu wengine.
Kwa mfano, virusi vya SARS-CoV ambavyo vilitokana na paka na virusi vya MERS-CoV ambavyo vilitokana na ngamia. Chanzo cha kuthibitisha kuwa COVID-19 inaweza kusambazwa na wanyama bado hakijathibitishwa.
Ili kujilinda, ni muhimu kama vile wakati wa kutembelea masoko ya wanyama hai, epuka kugusana moja kwa moja na wanyama haswa sehem za uso.
Beba nyama mbichi, maziwa au viungo vya wanyama kwa uangalifu ili kuzuia uchafuzi wa vyakula visivyopikwa na epuka kula bidhaa za wanyama mbichi au zilizochomwa.
Source: WHO