Home Elimu MSAADA WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA WAWASILI TANZANIA

MSAADA WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA WAWASILI TANZANIA

0 comment 120 views

Waziri wa Afya,Umy Mwalimu,ameeleza kuwa msaada wa vifaa tiba vya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Vifaa hivyo vimetolewa na mfanyabiashara maarufu wa nchini China,Jack Ma ambavyo vilifikia nchini Ethiopia kwa ajili ya kuvisambaza katika nchi zote 54 za Africa.Vifaa hivyo ni barakoa,vifaa vya kupimia na suti za kujilinda na maangamizi.

Waziri Mwalimu,kupitia kwenye mtandao  wa Twitter ameeleza kua ndege hiyo imefika usiku wa kuamkia leo na amemshukuru Ma pamoja na Serikali ya Ethiopia ambayo iliyopokea mizigo hiyo.

Ubalozi wa China nchini Tanzania, umesema vifaa hivyo ni Barakoa 100,000,suti za kujilinda 1,000 na vifaa vya upimaji 20,000.

Hadi sasa idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imefikia 24 na wengine wamepimwa na kugundulika hawana tena virusi vya Corona.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter