Home Elimu JE UNA TATIZO LA MATUMIZI MABAYA YA PESA?ZINGATIA HAYA

JE UNA TATIZO LA MATUMIZI MABAYA YA PESA?ZINGATIA HAYA

0 comment 151 views
Njia pekee ya kutunza pesa ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima Unachohitaji ni kujua pesa unatumia 
zaidi kwenye nini,hapo ndipo utakapojua ufanye nini ili kupunguza matumizi.
Kila mara weka akilini kuwa yawezekana unanunua kitu kwa bei rahisi lakini jiulize ufanisi wake una umuhimu wowote au ni kutimiza wajibu tu.
Tambua mahitaji yako halafu fanya hesabu za namna ya kutumia unachokipata kwa uangalifu.
Tambua kuwa
 ili kupunguza matumizi kufanikiwe ni lazima ubadilishe mfumo wako wa maisha na namna unavyofikiria.Zifuatazo ni hatua unaweza kuzitumia kupunguza matumizi:
1.TAMBUA UNATUMIA PESA ZAKO KATIKA NINI ZAIDI
Kama mpaka sasa hujui pesa zako unazitumia zaidi kwenye nini zoezi hili litakushinda.Ukiwa hujui pesa yako
unatumia kwenye nini hasa,kila mara utakuwa mtu wa kushangaa tu kuwa hela yako imepungua.Na wengine wanaweza kuwalaumu watu wako wa karibu kuwa wamewachukulia kumbe ni yeye mwenyewe ndiye aliyefanya matumizi.
2.EPUKA MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA
Kuna matumizi mengine hata wewe unayaona kabisa kuwa hayana ulazima lakini kwa kuwa ushazoea ndio unaona ni kitu cha kawaida.Na hivi ndio vitu mbavyo unanunua hapa baada ya dakika tano ukimaliza kukitumia ushasahau kama hata ulitumia.
 
3.WEKA KIPAUMBELE CHA UNUNUZI
Weka mkakati wa muda mfupi wa kutunza pesa unayopata kwa ajili ya kununua kitu fulani ndani ya muda uliojiwekea. Kama kuna kitu unataka kununua ijue bei yake halafu anza mkakati wa kutunza pesa kwa ajili ya kukimiliki.Hii itakusaidia kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.
4.PUNGUZA MATUMIZI YA SIMU
Mawasiliano siku hizi ndio yamekuwa yanaongoza kwa matumizi makubwa ya pesa.Ukiwa hujui muda gani  wa kupiga, na muda gani wa kutuma meseji utakuwa unajimaliza mwenyewe.Unaweza ukaweka vipaumbele vya watu wa kuwasiliana nao.Kama unafanya simu za biashara ni kitu kizuri lakini kama ni stori tupu hapo lazima ujizuie.
5.TENGENEZA ORODHA YA VITU VYA KUNUNUA
Unapoamua kuwa unataka kwenda kununua vitu fulani ni lazima uwe na orodha maalumu itakayokuongoza ili
usitumie zaidi ya uliyopanga.Usijiroge ukatoka nyumbani kwenda kununua vitu huku hujui nini hasa unaenda kununua na gharama yake ni shilingi ngapi?Utakuja kujuta wakati ushafikia nyumbani ukiwa huna pesa kabisa.
PESA INAYOTUMIKA TU BILA KUJIONGEZA NI SAWA NA KUJIFILISI MWENYEWE.
ANZA LEO KUTUNZA KIDOGO UNACHOPATA ILI KESHO USIJE KUJILAUMU 
ZITAKAPOKWISHA KABISA.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter