Home Elimu JE UNAWEZA UKAUGUA CORONA MARA MBILI?

JE UNAWEZA UKAUGUA CORONA MARA MBILI?

0 comments 155 views

Baadhi ya wagonjwa wamepona virusi vya Covid-19, baada ya vipimuo kuonesha kuwa hawana coronavirus, lakini je wanaweza kupatikana na virusi vya Covid-19 baadae?.

Maambukizi ya coronavirus, ambayo yanadalili kama ya mafua ya kawaida, kwa kawaida husababisha mgonjwa kuwa na kinga ya mwili.Je kuna tofauti na virusi hivi?

Mwanaume wa miaka 70 na zaidi ni mfano wa awali wa wagonjwa waliowapa madaktari uvumbuzi uliowatia hofu.

Alikuwa ametengwa katika chumba cha hospitali mwezi wa Februari baada ya kubainika kuwa na coronavirus.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Japan NHK, alipona na kurejea katika maisha yake ya kawaida, hata akatumia usafiri wa umma.

Lakini baada ya siku kadhaa akaugua tena na alikua na joto la juu la mwili.

Mwanaume huyo alirejea hospitalini na ilichomshangaza daktari,pale baada ya kufaniwa vipimo alibaini kuwa alikuwa na virusi vya corona tena.

Ingawa sio kisa pekee cha aina hiyo kilichopatikana nchini Japan, kwa sasa maambukizi yanayojirudia miongoni hutokea katika watu wachache, lakini ni visa muhimu. Lakini ni kwanini?

Kurejea tena kwa virusi baada ya kupona

Luis Enjuanes, mtaalamu bingwa wa virusi katika kituo cha taifa cha Uhispania cha teknolojia ya vimelea (CSIC), ameiambia BBC kuwa takriban 14% ya wagonjwa ambao hawajapatikana na Covid-19 baada ya kupimwa, baadae wanapopimwa tena hupatikana maambukizi ya coronavirus.

Anaamini haya sio maambukizi ya kwanza, bali ni kisa cha virusi “kurejea tana”.

“Maelezo yangu, miongoni mwa mengine mengi, ni kwamba kwa ujumla hii coronavirus inatengeneza kinga ya umma, lakini kinga hiyo sio thabiti kwa baadhi ya watu binafsi ,” Enjuanes anasema.

“Wakati kinga ya mwili inaposhindwa kuwa ya kutosha, baadhi ya virusi, ambavyo vinasalia katika hifadhi mwilini, huwa vinarejea.”

Virusi vinaweza kuishi katika mwili

Baadhi ya virusi vinaweza kuendelea kuishi ndani ya mwili kwa miezi mitatu au hata zaidi.

“Wakati mtu anapopatikana na virusi halafu baadae anapatikana kuwa hana baadae, dhana ni kwamba ametengeneza kinga ya mwili, kwa hiyo virusi havipaswi kujitokeza tena, kama ilivyo kwa vimelea vingine ,”anasema Enjuanes.

“Lakini baadhi ya virusi vya maambukizi vinaweza kuwa vipo ndani ya nyma za mwili ambazo hazijafikiwa na kinga ya mwili, sawa na sehemu nyingine za mwili.”

Lakini kuna kitu fulani kuhusu ugonjwa wa Covid-19 ambacho kinaendelea kuwashangaza wanasayansi ni: kipindi kifupi baina ya pale mgonjwa anapatwa na virusi tena na baada ya kupona.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!