Home AJIRA TOFAUTI KATI YA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA

TOFAUTI KATI YA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA

0 comment 139 views

Watu wengi wanachanganya kati ya hawa Wawili, leo tuone kidogo tofauti zao.

Wakati mfanyabiashara anatafuta Biashara inayolipa kwa kuangalia biashara zilizokwishafanywa hapo kabla, ambazo zinaendelea, au zile ambazo watu husimulia sana kuwa zinalipa, Mjasiriamali yeye hubuni wazo jipya kwa kuangalia matatizo yalioizunguka jamii ili kuyatatua na hiyo ndio fursa yake.
Mfanyabiashara mara nyingi hawezi kuvumilia hasara kwa lengo la kutengeneza faida kubwa baadae, na ndio maana wakianza biashara hufunga mapema mno, Mjasiriamali yeye anauwezo wa kuvumilia hasara mpaka lengo la msingi litimie, na wengi wamefanikiwa kwa kuvuka changamoto.
Wakati Mjasiriamali anafikiria namna ya kubuni biashara mpya, bidhaa mpya , Huduma mpya au kuboresha iliyopo kwa kuweka ubunifu, Mfanyabiashara yeye huangaika na kukopi kazi na biashara za wengine.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter