Home BIASHARA Kanuni 5 za Ujasiriamali Muhimu kuzifahamu

Kanuni 5 za Ujasiriamali Muhimu kuzifahamu

0 comment 89 views

Wengi hutamani au hata kujiingiza kwenye ujasiriamali, lakini siyo wote wanaofanikiwa kutokana na kutokufahamu kanuni muhimu za ujasiriamali. Ni wazi kuwa ili uanzishe kitu chochote chenye mafanikio, ni lazima ufahamu kanuni za kukifanya kitu hicho jinsi ipasavyo.

Ikiwa wewe ni mjasiriamali, au unataka kuwa mjasiriamali, basi fuatilia somo hili kufahamu kanuni 5 ujasilimali.

1. Kuwa mtatuzi wa matatizo

Ujasiriamali ni zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa mtu husika. Ni muhimu ukafahamu kanuni hii kama mjasiriamali kwani hutojikita kutafuta pesa bali utajikita kutatua matatizo ya watu.

Kwa mfano kama kuna tatizo la upatikanaji wa mboga katika mji au eneo unalokaa, ikiwa wewe utaleta mboga katika eneo hilo ni wazi kuwa watu watakupa pesa ili uwape mboga. Hivyo ni muhimu kila mara ukatafuta changamoto ukaitatua, nawe bila shaka utapata pesa za uhakika.

“Pesa ni matokeo ya kutatua shida ya mtu”

2. Kuwa na maono

Hakuna ujasiriamali bila maono. Kuwa mjasiriamali bila maono ni sawa na kuendesha gari isiyokuwa na usukani. Maono katika ujasiriamali yatakuwezesha kukuongoza ufanye nini na kwa muda gani. Ni lazima ujiulize kuwa unataka kuwa nani, lini na unataka kufanya nini baadaye? Jonathan Swift alisema maono ni sanaa ya kuona kile ambacho wengine hawaoni. Ni lazima uwe na lengo na ufanye bidii kulifikia.

“Wajasiriamali waliofanikiwa ni wale walioweza kubadili maono yao kuwa uhalisia”

3. Chagua washirika au timu sahihi

Wakati mwingine utahitaji kufanya kazi na watu au mtu fulani. Ni muhimu kuwa makini wakati wa kuchagua washirika au timu ya kufanya nayo kazi ili kuhakikisha maono yako hayakwamishwi. Kamwe usichukue mtu tu kwa kigezo kuwa ni rafiki au ndugu yako, bali chukua mtu ambaye unaamini anaweza kufanya kitu chenye tija kwa ajili ya kufanikisha malengo yako kama mjasiriamali.

4.Toa huduma au bidhaa yenye tija

Hivi leo sokoni kuna bidhaa na huduma nyingi ambazo ni za aina moja, lakini siyo zote zinafanya vizuri. Hii ni kutokana na baadhi ya bidhaa au huduma kutozingatia kuwa na tija kwa wateja wake. Ikiwa unatengeneza bidhaa au huduma fulani hakikisha itakuwa na manufaa makubwa na ya uhakika kwa wateja wako.

Kwa mfano nimewahi kuona vitafunwa vilivyoandaliwa katika mazingira duni na kuwa na dosari mbalimbali kama vile marashi, vipande vya nywele, mchanga n.k. Ni wazi kuwa bidhaa za namna hii zitakosa wateja kutokana na kuwa na ubora duni. Kila mara kumbuka kuwa ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuongeza tija na ubora wa huduma na bidhaa zako.

5. Tumia pesa vyema

Changamoto ya matumizi mabaya ya pesa inawakabili watu wengi kuanzia kwenye matumizi yao binafsi ya pesa. Watu wengi wanapata pesa lakini zinaisha bila ya kufahamu wamezitumiaje au wamefanya kipi chenye tija.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter