Home BIASHARAUWEKEZAJI Rais Mwinyi ataka orodha ya wawekezaji Zanzibar

Rais Mwinyi ataka orodha ya wawekezaji Zanzibar

0 comment 203 views

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kumpatia orodha ya wawekezaji visiwani humo.

Dk. Mwinyi alitoa maelekezo mbalimbali kwa mamlaka hiyo ili kuhakikisha inafanya kazi kwa ufasini na kuvutia wawekezaji.

Ameutaka uongozi wa ZIPA kumpatia majina ya wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza Zanzibar pamoja na thamani ya miradi wanayotaka kuwekeza na changamoto wanazokutana nazo katika uwekezaji ili watafute namna ya kuzitatua.

Raisi Mwinyi alitoa maelekezo hayo wakati alipofanya mazunguzo na Uongozi wa ZIPA katika Ukumbi wa Ikulu Zanzibar.

Dk Mwinyi, ameiweka wizara ya Uchumi na Uwekezaji chini ya ofisi ya Raisi ili kuhakikisha uwekezaji unakua visiwani humo.

Aliitaka Mamlaka ya uwekezaji kubadili mfumo wa ufanyaji biashara kama wanataka kukuza uwekezaji na kufutia watalii.

Pia aliitaka ZIPA kushughulikia urasimu ambao unasumbua wawekezaji na kuwafanya kuacha ama kusimamisha miradi mbalimbali waliokuwa wakiifanya.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter