Home BIASHARA Waziri Dk. Ndugulile aitaka TTCL kuacha kufanya biashara kwa mazoea, aipongeza

Waziri Dk. Ndugulile aitaka TTCL kuacha kufanya biashara kwa mazoea, aipongeza

0 comment 143 views

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile amelitaka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kutofanya biashara kwa mazoea.

Waziri Ndugulile, pia amelipongeza shirika hilo kwa kujiendesha kwa faida na kupunguza hasara kwa kipindi cha miaka mitano.

Dk. Ndugulile ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha utendaji kazi wa Mameneja wa TTCL Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar na Menejimenti ya Shirika hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi la Zimamoto.

“Ongezeni ubunifu ikiwamo kufanya utafiti wa masoko ili kubaini mahitaji ya wateja, kuongeza wateja na kwenda sambamba na ushindani.

Mpaka sasa TTCL ina asilimia mbili ya wateja wa simu za mkononi kwenye soko ukilinganisha na kampuni nyingine na jumla ya wateja milioni 1.3 wa simu za mkononi,” amesema Dk. Ndugulile.

Aliongeza kuwa “mmefanya kazi nzuri sana mimi niwapongeze, kutoka kujiendesha kwa hasara mpaka kuja kwenye faida hili ni jambo la kupongezwa kwa TTCL, niwatake sasa muongeze nguvu na kuacha kufanyabiashara kwa mazoea.

Aidha, katika kikao hicho mameneja hao pia walijadili na kuweka malengo yanayopimika kwa kuwa hivi sasa kiasi cha Sh trilioni 12 kinazunguka kwenye huduma ya fedha mtandao kwa mwezi na miamala isiyozidi milioni 300 kwa mwezi inapita mtandaoni ili TTCL itumie fursa hiyo kufanya biashara na kutoa gawio.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alimemweleza Dk. Ndugulile kuwa Shirika lake limeweza kujiendesha kwa faida kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2016/2017 kwa kutengeneza faida ya Sh bilioni 5 kwa mwaka tofauti na miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2016 ambapo Shirika lilikuwa likijiendesha kwa hasara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter