Ukuta uliojengwa kuzunguka eneo la mgodi wa Tanzanite, Wilayani Simanjiro, mkoa wa Manyara, umewezesha mapato ya serikali kuongezeka kutoka Sh milioni 238 mwaka 2016 kufikia Sh bilioni 1.417 mwaka jana.
Prof. Saimon Msanjila ambae ni Katibu Mkuu Wizara ya Madini amesema ukuta huo ambao pia umezungukwa na kamera za CCTV umepunguza utoroshwaji wa madini uliokuwa ukiinyima serikali mapato na kudhibiti ajira kwa watoto mgodini hapo.
Ukuta huo una urefu wa kilometa 24.5 umejengwa baada ya Rais Magufuli kutoa agizo la ujenzi huo Septemba mwaka 2017 ili kudhibiti na kuzuia utoroshaji wa madini ya Tanzanite.