Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa ya Meiy 07 anatarajiwa kufanya mkutano na zaidi ya wazee 900 wa mkoa wa Dar es salaam ambapo Katika kikao icho watajadili mambo mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amesema kikao hicho kitafanyika katika Ukumbi wa Mikutano Mlimani city kuanzia saa 8 Mchana.
Aidha RC Kunenge ametoa wito kwa Wazee waliopata mialiko ya kushiriki kikao icho kujitokeza kwa wingi ili wapate kujua kile ambacho rais Samia amewaitia.
Kwa upande wao Viongozi wa Wazee wamemshukuru rais kwa kuona umuhimu wa kukutana nao na kusema wanatarajia kikao hicho kitakuwa cha manufaa makubwa kwao.