Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amesema Serikali imejifunza kupitia moto uliotokea Karikaoo na kusema kuanzia sasa masoko yote makubwa yanayomilikiwa na Halmashauri na Stendi kubwa wakianzia na Stendi ya Magufuli iliyopo Mbezi, zitawekwa vifaa vya kuzimia moto pamoja na visima vya maji ili kukabiliana na majanga ya moto.
“Masoko yote yanayomilikiwa na Halmashauri zetu, hususani Masoko makubwa, Stendi zetu zote ambazo zinamilikiwa na Halmashauri zetu tutahakikisha zinakuwa na visima vya maji, ili kuweza kukabiliana na majanga haya ya moto”
Waziri Ummy ametembelea soko la Kariakoo ambalo liliungu juzi usiku na amesema taarifa za awali zinaonesha wafanyabiashara 224 ni wahanga wa janga la moto uliotokea sokoni hapo juzi usiku.
hilo.
“Tunasubiri taarifa ya uchunguzi ya Tume ya Waziri Mkuu, pia tumepokea taarifa, kuna wengine mali zao zimepotea/kuibiwa.” Amesema Waziri Ummy
Ametoa pole kwa wafanyabiashara wote na kuupongeza uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam chini ya RC Amos Makalla kwa jinsi walivyoitikia kwa haraka kushughulikia janga hilo.