Uwepo wa Wakala wa Vyuo Vikuu vya Nje imekuwa ni msaada mkubwa kwa wanafunzi wanaohitaji kusoma nje ya nchi zao.
Wakala hawa ambao kazi yao kubwa ni kuwasaidia kufanya mchakato mzima wa wanafunzi na watu wanaohitaji kwenda kusoma nje ikiwemo kuchagua chuo, kozi na hata upatikanaji wa viza.
Darwin Education Agency Limited ni moja ya mawakala wa Vyuo Vikuu vya Nje wanaofanya shughuli zake Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Darwin, Joseph Makungu anasema wamekuwa wakifanya uwakala nchini Tanzania tangu mwaka 2015.
“Tumesajiliwa na tume ya Vyuo Vikuu ambapo tunawasaidia watu kuwapa ushauri wakielimu ni namna gani mwanafunzi achague kozi kawa ngazi mbalimbali za elimu kuanzia Astashahada, Stashahada, Shahada na kuendelea” Ameeleza.
Amesema kwa mwaka huu wamepeleka wanafunzi zaidi ya 15 ambao wamepata udhamini wa kila kitu ikijumuisha ada, malazi na chakula.
“Bado tuna nafasi za udhamini kwa kozi mbalimbali, wale wanafunzi ambao wapo kidato cha sita wanaweza kufanya maombi yao mapema kuanzia Disemba wanaweza kubahatika kupata udhamini” amesema.
Rachel Mbajo ambae ni afisa masoko wa Darwin amesema mwitiko kwa sasa ni mkubwa tofauti na hapo awali.
Ameeleza kuwa wameingia mkataba na nchi mbalimbali ikiwemo India, China na Cyprus ambao hutoa udhamini kwa wanafunzi.