Home BIASHARA EWURA yatangaza ongezeko la bei ya mafuta

EWURA yatangaza ongezeko la bei ya mafuta

0 comment 164 views

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa bei za mafuta zimeongezeka ambapo bei ya petroli imeongezeka kwa asilimia 23 kutoka dola za Marekani 644.01 kwa tani kwa mwezi Mei 2021 na kufikia dola 793.14 mwezi Oktoba 2021.

Kwa kipindi hicho, bei ya petrol katika soko la ndani zilipaswa kuwa zimeongezeka kwa jumla ya Sh. 241 kwa lita na kufikia Sh. 2,610 kwa lita mwezi Disemba 2021.

Bei ya dizeli nayo imeongezeka kwa asilimia 30 kutoka dola za Marekani 550.68 kwa tani mwezi Mei 2021 na kufikia dola za Marekani 713.28 kwa tani mwezi Oktoba mwaka huu.

EWURA inasema kwa kipindi hicho bei ya dizeli katika soko la ndani zilipaswa kuwa zimeongezeka kwa jumla ya Shilingi 311 kwa lita na kufikia Shilingi 2,492 mwezi Disemba 2021.

Kwa upande wa mafuta ya taa bei imeongezeka kwa asilimia 30 kutoka dola za Marekani 558.90 kwa tani kwa mwezi Mei 2021 na kufikia dola za Marekani 726.56 kwa mwezi Oktoba 2021.
Bei ya mafuta ya taa katika soko la ndani zilipaswa kuwa zimeongezeka kwa jumla ya Shilingi 120 kwa lita na kufikia Shilingi 2,235 mwezi Disemba mwaka huu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter