Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema daraja la Tanzanite Watanzania hawalipi na hawatalipa kwa sababu limejengwa kwa 100% kwa pesa ya serikali.
Waziri Mbarawa amebainisha kuwa fedha hizo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Korea Kusini ambazo zitalipwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia zote.
“Daraja la Kigamboni utaratibu uliotumika ni tofauti, pale serikali iliingia makubaliano na NSSF kwa ajili ya uwekezaji ule.
Na baada ya NSSF kuwekeza ile pesa lazima irudi. Na ndio tukakubaliana kwamba pale daraja lile watu watalipa tozo ndogo ili waweze kuchangia katika kurejesha pesa iliyotumika na NSSF” amesema Waziri.
Ameeleza kuwa huo ndio utaratibu na utaratibu huu unatumika maeneo mengi duniani sio hapa Tanzania tuu.
Daraja la Tanzanite(Salenda) lilianza kutumika rasmi February Mosi, 2022.
Soma: Ujenzi daraja la Tanzanite wakamilika