Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Maandamao mfumuko wa bei yamtia matatani Kizza Besigye

Maandamao mfumuko wa bei yamtia matatani Kizza Besigye

0 comment 114 views

 

Kampala. Mwanasiasa ambae pia amewahi kugombea nafasi ya urais mara nne nchini Uganda Dk. Kizza Besigye amekamatwa na polisi nchini humo.

Besigye amekamatwa baada ya kujaribu kurudisha maandamano yenye jina “Muzuukuke” ikimaanisha “amka” leo Mei 23 asubuhi.

Maandamano hayo yanatokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Kabla ya kukamatwa, kiongozi huyo wa upinzani alikuwa akizungumza na vyombo vya habari akielezea mfumuko wa bei nchini humo akisema serikali haijatoa suluhisho la tatizo hilo.

Besigye, ameelezea mazungumzo ya Rais Museveni kwa vyombo vya habari Jumapili juu ya hali ya uchumi nchini humo kuwa ni “mazungumzo matupu”.

“Tupo peke yetu, hivyo tunatakiwa kutafuta suluhu ya hili tatizo linalotukabili, Waganda mnatakiwa kuamka,” amesema Besigye.

Wakati akizungumza na vyombo vya habari, polisi walikuwa nje ya geti la nyumba yake na hawakumpa nafasi ya kuondoka.

Mara baada ya kukamatwa kwake, wafuasi wa Besigye wametumia mtandao wa kijamii wa Twitter wakisema polisi wanafanya kazi kama wahalifu na kusisitiza kuwa kukamatwa kwake kutaleta madhara.

“Holding him at home will not solve the economic crisis we face, a crisis started by Mr. Museveni regime. No turning back. Muzuukuke campaign continues,” the Front said in a tweet.

“Kumshikilia nyumbani kwake sio suluhu ya janga la kiuchumi tunalokumbana nalo,” wameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wakilaumu utawala wa Rais Museveni.

Naibu msemaji wa polisi mji wa Kampala  Luke Owoyesigyire amesema kuwa Besigye hayupo chini ya ulinzi lakini amezuiwa baada ya kuzozana na maofisa wa polisi.

“Hayupo chini ya ulinzi lakini tunafuatilia nyendo zake,” amesema.

 

Chanzo: Nile Post News

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter