Home BIASHARA Rais Samia apokea Kombe la Dunia

Rais Samia apokea Kombe la Dunia

0 comment 110 views

Rais Samia Suluhu Hassan leo Mei 31, 2022 amepokea Kombe la Dunia la Mashindano ya Mpira wa Miguu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akipokea kombe hilo Rais Samia amesema kombe hilo kutembezwa Tanzania kuna maana kubwa kwenye mchango wa kiuchumi na kijamii kwa fursa zinazoweza kupatikana katika kuitangaza nchi.

“Kwa maneno mengine hapa Tanzania tunasema huyu ni mwali, kwa hiyo kabla hajaenda kufunguliwa anakopelekwa sisi tumepata fursa ya kumuona. Na ingekuwa ni bi. Harusi hao wanaooa wangepigana sana, kwa nini bi harusi wao mnamtizama kabla wao hawajamfungua,” amesema Rais Samia.

Ameishukuru Coca Cola na kusema hiyo ni heshima kubwa kwa kombe hilo kuletwa Tanzania.

Rais amemshukuru balozi wa Qatar na kusema “tumshukuru balozi ambae leo yupo nasi akilisindikiza kombe hili na akilitupia jicho kwa vizuri zaidi tusije tukalitia doa likafika Qatar lina vidotodoto, tutajitahidi kulitunza lifike salama.”

Ameitaka Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kuwekeza zaidi kwenye michezo.

Amewahamasisha watu kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa taifa kuliona kombe hilo.

Amewataka watanzania kutumia mashindano hayo kuitangaza fursa zilizopo nchini ikiwemo utalii na uwekezaji.

Ameshukuru kampuni ya Coca Cola kwa kuwapatia Watanzania fursa ya kuliona kombe hilo kabla ya kwenda kufunguliwa huko Qatar.

Tanzania ni miongoni mwa mataifa tisa Afrika ambayo yanatembelewa na kombe hilo la mwaka huu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter