Fursa imetolewa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kutangaza na kuuza bidhaa za Tanzania katika soko la China kw njia ya mtandao wa JD Worldwide Cross Border E-Commerce Platform.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imetangaza fursa hiyo kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini China.
Taarifa ya TanTrade kwa wafanyabiashara inawataka kuwasilisha taarifa zao za bidhaa zinasokodhi ubora wa limataifa (content & package) pamoja na viwango vinavyokubalika katika soko hilo.
“Tunaalika kampuni mbalimbali za Tanzania zenye nia ya kuuza bidhaa katika soko lwa mtandao la China kuwasilisha taarifa zao,” inasema taarifa hiyo.
TanTrade imetaja bidhaa zitakazopata kipaumbele kuwa ni pamoja na vyakula vilivyochakatwana bidhaa zilizotayari kutumika ambazo ni matunda yaliyokaushwa, kahwa, korosho, chai, viungo, asali vito vya thamani (madini) na sanaa na utamaduni.
Nyingine ni bidhaa za ngozi, mkonge, mbao, moringa na pamba.
Mtandao huo unatumiwa na zaidi ya watu milioni 700 nchini China.